Ofisa habari wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amewataka mashabiki wa Simba kutokwenda na matokeo yao mfukoni kesho uwanja wa taifa kwa kuwa watakachokipata kitawashangaza.
Bwire amesema wamejipanga kuonyesha mchezo ambao wengi hawajawahi kuuona, wamezipata mbinu zote za Simba hawaoni ugumu wa kupata matokeo katika mchezo huo.
"Tunawaomba mashabiki wasije na matokeo mkononi watakachokipata kitawashangaza, wanapaswa wawe watulivu tutakavyowapapasa bila shida yoyote ile.
"Wengi hawaipi uzito Ruvu Shooting kufanya vizuri, lengo letu ni kuhakikisha tunatambulika, tunakuja na mfumo mpya ambao utafanya kazi, nawapa pole Simba kwa sababu watu watachanganyikiwa," alisema.
Tangu simu wa 2013/14 Simba imekutana na Ruvu Shooting mara nane kwenye ligi Kuu Bara katika michezo hiyo Simba imeshinda mara saba na wametoka sare mara moja.
Utaaibika kaa kimya ww simba lazima akunga'ate.
ReplyDeletemasau acha kutupiga mkwala wa mbu nje ya net leo tunakupiga 7 tena
ReplyDelete