October 28, 2018


Mashabiki wa timu ya Simba wamepokea matokeo ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo wa ligi kuu uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya mchezo Ofisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisema ana uhakika wa kupata matokeo kutokana na kuja na mfumo mpya ambao ungewashangaza mashabiki na kuweza kuchanganyikiwa kwa kupata matokeo ambayo hawakutarajia.

Mchezo ulivyoanza, Bwire alikuwepo Uwanjani katika viti vya watu maalum, VIP ,Okwi alipoanza kuandika bao la kwanza dakika ya 7 bado alikomaa akiamini wana nafasi ila bao la tatu lilipofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 56 hakuoneka tena mpaka mchezo unaisha.

Mashabiki waliendelea kumtafuta kwa jitihada baada ya kuisha mchezo hawakufanikiwa kumuona mzee wa kupapasa Square ambaye kibao kimemgeuka leo kwa kukubali kufungwa mabao 5-0. 

Ushindi huo unawarejesha kwenye reli Simba baada ya kucheza michezo 10 wamefanikiwa kujikusanyia jumla ya pointi 23.

4 COMMENTS:

  1. Simba wameanzia mbali,kwanza nagoli aina ya gari lisilo na matairi, yaani hawafungi, baadae magoli ya wilbarrow yaani goli moja, yamekuja magoli ya matairi ya pikipiki, baadae ya kibajaji, hatimae yamekuja magoli ya matairi ya taxii, sasa tunasubiri ya magoli ya semitrella, tutayapata?

    ReplyDelete
  2. Ndio maana time inatakiwa kuwa yenye uwezo was kifedha ili kujiendesha, Simba imeweza kusajili wachezaji wengi wenye vipaji tofautifauti, katika hao huwezi kukosa kupa matokeo chanya, kwa mwenendo huu was sasa tunategemea matokeo chanya tu, zile nyakati za kwamba baba yangu alipiga matofali kuijenga klabu hii ziishapita, tutafute kusonga mbele kwenye mafanikio ambayo kila MTU anayahitaji, wale waaanilishi watawekwa kwenye ubao maalumu utakao watambulisha hivyo kuwa walikuwa na wazo bora nasi tumelifikisha hapa, simba tunataka tuwe was kwanza kuleta kombe LA Afrika Tanzania, so was ushindani na wapiga kelele kwenye masoko na magenge! Nawapa bigup Simba ninayoipenda, kwa sasa nipo tayari kuwa nwanachama kwa Mara nyingine, tunahitaji magoli ya semitrailor sasa ili wasema hovyo wanyamaze na kufunga midomo yao michafu kwa maneno.

    ReplyDelete
  3. Ndio maana naipenda timu yangu hii ya Simba. Inanipa raha sana. Ule mpira hata unavyochezwa, burudani inaonekana jinsi inavyoingia hadi Moyoni. Nina uhakika kama sio kukosa utulivu kwa Boko na Kagele, jana Masau Bwire angeondoka na furushi la magoli kumi. Kwa hali hii, Mpira ungekuwa ni siasa halafu timu ni vyama, nina uhakika jana au leo tungewapokea wanachama wengi sana hususani wale jirani zetu wa bwawani, wakirudisha kadi zao na kuchukua kadi za Simba. Big up kwa wote waliochangia mwendelezo huu wa ushindi mnono. Wasioipenda Simba wafeeeeeeeeeeeeeeee.............. tutabaki wenyewe na raha zetu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic