Bwire alisema kuwa anakuja na mbinu ambayo ingeushangaza ulimwengu kwa kuweza kuwafunga mabingwa hao watetezi na kuwafanya waulize wanakokaa hali ambayo iliwafanya viongozi wa Simba kutulia.
Ofisa wa habari wa Simba Haji Manara kabla ya mchezo alisema kuwa atamjibu Bwire ndani ya Uwanja kwa kuwa anaamini timu yake ni kubwa na itafanya maajabu na imedhihirika baada ya mchezo kuisha.
"Tumecheza mchezo na tumedhihirisha kwamba sisi ni mabingwa, Okwi ni mchezaji bora na maarufu zaidi wa kigeni Tanzania toka Uhuru, anaogopwa zaidi na wapinzani wetu." alisema.
Katika michezo tisa waliyokutana Simba na Ruvu Shooting tangu msimu wa 2013/14, Simba imeshinda michezo nane na wamelazimisha sare mara moja tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment