Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa kiingilio cha Sh 2,000 kwa mechi ya kesho Taifa Stars ikiivaa Cape Verde ni sahihi.
TFF imesema inaamini kiingilio hicho ni kizuri na wananchi asilimia kubwa wataweza kulipa kuiona timu yao ikipambana.
Msemaji wa TFF, Cliford Ndimbo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi na kuisaidia Stars.
“Tunaamini kiingilio ni kizuri kabisa, tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu.
“Kuhusiana na maandalizi, yamekuwa ni mazuri na morali iko juu. Vijana wamepania kufanya vizuri,” alisema.
Katika mechi iliyopita, Stars ilipoteza mechi yake kwa kulala kwa kufungwa mabao 3-0 mjini Praia.







0 COMMENTS:
Post a Comment