October 27, 2018


Meneja wa Yanga Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye alikuwa nahodha wa zamani ndani ya kikosi hicho jana alifanyiwa 'sapraiz' ya aina yake kutoka kwa mashabiki wa Yanga wa kijiji cha Chigugu kilichopo Mtwara.

Mashabiki hao walikuwa barabarani kusubiri msafara wa Cannavaro uliokuwa unaenda kufungua tawi la Yanga mkoani Mtwara.

Msafara huo ukiwa njiani ulisimamishwa na mashabiki hao ambapo wazee wa eneo hilo walimkabidhi Cannavaro katoni nne za maji huku wakimwambia akirudi apitie kuchukua kuku wake kama zawadi.

Yanga wamekuwa na matokeo mazuri msimu huu kwani katika michezo 8 waliyocheza wamefanikiwa kushinda saba na kutoa sare mchezo mmoja huku wakiwa na pointi 22 na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

7 COMMENTS:

  1. Kitaeleweka tu pale watakapo anza kupigwa mfululizo.

    ReplyDelete
  2. Hata simba na azam hazijawah fungwa kwao tangu msimu huu ulipoanza,kwakifupi wajipange kisawa sawa watapigwa sana.

    ReplyDelete
  3. Hata simba na azam hazijawah fungwa kwao tangu msimu huu ulipoanza,kwakifupi wajipange kisawa sawa watapigwa sana.

    ReplyDelete
  4. Basi, mwandishi aseme Yanga iliyopoteza mechi 3 mfululizo ikiwa nyumbani.

    Ili mfurahi, maana taarifa za ukweli zinawauma. Basi muwekewe porojo Mfurahi.

    ReplyDelete
  5. Basi, mwandishi aseme Yanga iliyopoteza mechi 3 mfululizo ikiwa nyumbani.

    Ili mfurahi, maana taarifa za ukweli zinawauma. Basi muwekewe porojo Mfurahi.

    ReplyDelete
  6. Kikikubwa ni kuiandaa timu kimbinu na kiushindani, popote unashinda, mbona wanachezaji wa azam,Simba na yanga wanatokea ukouko mikoani,tuache kukariri mpira

    ReplyDelete
  7. Keya Saidi umepanic brother huko mikoani ni wapi??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic