October 7, 2018


Mwandishi, Mchambuzi na Mhariri Mkuu wa gazeti la Championi, Saleh Ally, amefunguka kwa kutoa mtazamo wake juu ya sakata linalomkabili Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma.

Ally ameeleza kuwa ifikie hatua sasa Simba vema wakabaki na mtu mmoja ili kuonda visingizio pale timu hiyo inaposhindwa kupata matokeo mazuri uwanjani.

Mchambuzi huyo ambaye pia ni Mhariri wa gazeti la Spoti Xtra linalotoka siku za Alhamis, na Jumapili, ameeleza kuwa endapo Djuma ataondoka Simba itakuwa ni maamuzi sahihi.

Kuondoka kwa Djuma kutaisaidia Simba kuondoa visingizio kutokana na baadhi ya wadau na mashabiki wa timu hiyo hivi karibuni kuujia juu uongozi wakiutaka kuendelea kumpa nafasi Mrundi huyo.

Hata hivyo Ally amesema hawezi kulizungumzia kinagaugaba suala hilo mpaka uongozi wa Simba utakapotoa tamko rasmi juu kuachwa kwake.

5 COMMENTS:

  1. Kaimu raisi wa Simba Try again ameeleza vizuri sana na kwa uwazi zaidi kuhusiana suala la Masoud Djuma. Masoud anataka kuwa kocha mkuu wa Simba na kuna madai ya baadhi ya vyombo vya habari au watu wanaodai kuwa Simba walimuahdi kuja kuwa kocha mkuu wakati simba wakisema wamemuajiri Masoud kuja kuwa kuwa kocha msaidizi kwa malengo ya kuja kumpandisha daraja ili aje kuwa kocha mkuu baada ya kupata uzoefu wa kutosha kutoka kwa makocha wakubwa watakaoletwa na club. Lakini inasemekana Masoud amekuwa akiwasaliti wakuu wake wa kazi kuanzia mkamerooni Omog na baadae mfaransa Lerchante kwa namna moja au nyengine ili kujitengezea ujiko kwa malengo ya kupewa ukocha mkuu wa Simba. Na inasemekana hata Mbeligiji katua Simba akiwa tayari na taarifa za tabia za msaidizi wake huyo mkononi alizozipata au kutoka kwa mzungu mwenzake aliemtangulia klabuni hapo. Inasemekana Mfaransa alieondoka Simba alifanya jitihada za kumuhabarisha mzungu mwenzake huyo juu ya tabia ya Masoud Djuma ingawa viongozi wa Simba walijaribu kuwafanya wawili hao kuwa kitu kimoja ila Masoud Djuma ikionekana kama kutoridhika na jitihada hizo za upatanishi kwa kutokuwa na ushirikiano wa dhahiri kwa mkuu wake wa kazi. Na kama kweli Masoud ana kiherehere hicho basi ni tatizo si kwa Simba tu hata kwa yeye mwenyewe binafsi. Subira ya vuta heri. Yeye mwenyewe aliwahi kusikikana akisema ana uwezo wa kufanya kazi hata ulaya ni vizuri kama ana uwezo huo ila kama kweli anamalengo ya kufundisha ulaya basi connection ndio hizi za wa hawa wazungu alitakiwa kujenga nao urafiki katika kazi ili kumpatia connection zaidi badala ya kuendeleza umimi. Hakika kama Masoud angekuwa mstaamilivu angekuwa tu kocha mkuu wa Simba siku moja pengine muda si mrefu. Simba wapo serious na ujenzi wa timu yao na wanaamini makocha wazoefu wa kiwango cha akina Lerchante na Patrick Ausems ni watu sahihi wa kuweka misingi ya Simba mpya. Na sio kama Simba hawaelewi uwezo wa Masoud Djuma wanaelewa ila kama Masoud angekuwa na ushirikiano wa dhati kwa wakuu wake wa kazi kutaka timu kufanikiwa basi SIMBA ni miongoni mwa Timu yenye benchi imara la ufundi kwa ukanda wetu huu wa Africa. Lakini kama watanzania, tukiacha na ushabiki kwa manufaa ya vijana wetu na timu ya Taifa basi tunapaswa kuona vijana wetu wakilelewa katika misingi bora ya soka kutoka kwa walimu wenye uweledi katika masuala ya nidhamu na team work. Ukiangalia hawa makocha wengi wa kigeni wanaokuja na kuondoka ni makocha wa viwango na wazuri ila watanzania tunahulka ya kutaka kupanda leo na kuvuna leo kamwe hatutafika kwa hulka za namna hiyo. Mfano mzuri ni kocha wa zamani wa Simba na sasa Gormahia Kerry, aliwezaje kuifanya Gormahia kuwa timu ya kitisha si Africa mashariki tu bali barani Africa lakini aliondoshwa Simba kuwa hafai?

    ReplyDelete
  2. Makocha wakuu mara nyingi ndio wanaopendekeza wasaidizi wao.

    ReplyDelete
  3. Kwanini tusitumie mfumo wa wenzetu walioendelea? Kwamba Kocha mkuu aje na wasaidizi wake.

    ReplyDelete
  4. Ni kweli Kocha mkuu anapaswa kuja na kocha msaidizi lakini Simba walimlewesha Aussems ili kumpa nafasi Masoud ya kujifunza na kuwa understudy ili apate nafasi ya kuwa kocha mkuu.Masoud ameonyesha udhaifu katika ushirikiano.Omog,Lechantre na sasa Aussems hawawezi wote kumzulia kuwa ana majungu na kupenda ukubwa.Simba wameonyesha uvumivu mkubwa kwa Masoud lakini enough is enough.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic