NIYONZIMA AIBUA JINGINE SIMBA, MBELGIJI AFUNGUKA
Kocha Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems, amewapa shavu wachezaji wake wawili, Haruna Niyonzima na Juuko Murshid kwa kusema huu ni muda wa wachezaji hao kucheza zaidi.
Niyonzima na Juuko walikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichocheza na African Lyon wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo Niyonzima aliingia dakika ya 77 huku Juuko yeye akiishia kukaa benchi kama mchezaji wa akiba.
Kocha huyo ameliambia Championi Jumatano, kwamba kwa sasa anataka kufanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kuhakikisha kila mchezaji anapata nafasi ya kucheza ikiwemo wachezaji hao wawili ambao wameingia kwenye timu katika kipindi hiki.
“Nina wachezaji wengi hapa na kila mmoja anahitaji kucheza kwa ajili ya kuongeza uwezo wake, ni muda sasa wa kufanya mabadiliko katika kikosi kwa kumpa nafasi kila mmoja na ndiyo maana utaona hata Niyonzima amepata nafasi kwenye mechi yetu hii.
“Jambo ambalo ninataka kufanya ni kuona kila mmoja anacheza kwenye mechi zetu ili kuwafanya wawe na uwezo wa hali ya juu, lakini sambamba na hilo ninahitaji pia kuboresha eneo langu la ushambuliaji,” alisema Mbelgiji huyo.
Sasa hapo kaibua nn
ReplyDeleteWaandishi wa kishamba. Wavumilie.
ReplyDelete