October 9, 2018


Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Soka ya Cameroon, Samuel Eto’o Phills anatarajia kutua nchini Jumatano ya wiki hii kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa Mpira wa Miguu utakaokuwa unamiliwa na kampuni ya Bia Tanzania –TBL.

Mbali na kuzindua uwanja huo huo Eto’o ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Chelsea ya Uingereza na Barcelona ya Hispania kwa nyakati tofauti atashiriki kuhamasisha vijana kuhusu michezo hapa nchini.

Pamela Kikuli ambaye ni Meneja wa Bia Castle na hapa anafafanua juu ya kampeni ya kuwaleta watu pamoja pia imezihusha Simba na Yanga.

Kwa upande wao wasemaji wa Simba na Yanga wamewapongeza castle lager kwa kusapoti maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic