Beki wa timu ya Simba Shomari Kapombe amekuwa mtamu kama Claytous Chama leo katika mchezo uliochezwa taifa dhidi ya Ruvu Shooting na kushuhudia Simba wakishinda kwa mabao 5-0.
Kapombe ametengeneza pasi za mabao 2 ambayo yalifungwa na Emmanueli Okwi na Chama pia alitengeneza pasi moja ya bao lililofungwa na Okwi ambaye alifunga 'Hat-trick' ya pili msimu huu.
Kapombe amekuwa katika mchezo mzuri leo akishirikiana na safu ya ulinzi kwa umakini kabisa alikuwa anapanda na kushambulia pia, dakika ya 43 alifunga bao baada ya kupigwa pasi kama zote kutoka kwa Chama kisha,Kagere, Okwi, Kapombe akatupia kwenye nyavu, mwamuzi akasema ameotea.
Chama ameendelea kuwa katika mwenendo mzuri kwa kuwa kila sehemu ambayo kulikuwa na mpira naye pia alikuwepo na amekuwa makini katika kumalizia pasi za mwisho hali ambayo imesaidia timu kucheza kwa kushambulia zaidi huku Ruvu Shooting wakicheza kwa kujilinda zaidi.
This is simbaaaaaaaaaaaa.jipangeni aseee kuna mtu atakuja chezea dazen nzima ya magoli.ngoja tuendelee kucheki burudani.
ReplyDeleteThis is simbaaaaaaaaaaaa.jipangeni aseee kuna mtu atakuja chezea dazen nzima ya magoli.ngoja tuendelee kucheki burudani.
ReplyDelete