October 10, 2018


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba raia wa Rwanda, Meddie Kagere amewaambia mashabiki kwamba ni mapema mno kumuhukumu kutokana na mechi chache alizocheza.

Kagere amefunga mabao manne hadi sasa kwenye ligi, ameshindwa kufunga bao lolote katika michezo mitatu iliyopita ukiwemo dhidi ya Yanga ambao mashabiki walikuwa wameweka matarajio yote kwake.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Kagere alisema; “Ni vyema nikaulizwa juu ya kuto­funga baada ya kumal­izika kwa ligi, kwa sasa bado nina safari ndefu kwenye ligi kuhakikisha naisaidia timu yangu ifanye vizuri, kipindi hiki sipo vizuri.

“Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa, tunahitaji kuisaidia timu yetu iweze kuwa vizuri kwani lengo letu ni kutwaa ubingwa,” alisema Kagere ambaye alisa­jiliwa na Simba akitokea Gor Mahia.

1 COMMENTS:

  1. Mungu atakusaidia uiongoze simba kuudhibiti ubingwa wake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic