October 10, 2018


Changamoto ya usafiri wa mabasi yaaendayo haraka (UDART) kutoka maeneo ya Kimara kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam imeendelea kuwakabili wakazi wa Kimara na Mbezi kutokana na mabasi hayo kuwa machache.

Kwa takribani siku tatu sasa, mabasi hayo yameshindwa kukidhi huduma hiyo kwa watumiaji wa usafiri huo hali inayosababisha msongamano mkubwa kwenye kituo cha mabasi hayo Kimara.

Mapema leo Oktoba 10 kituo cha Kimara kimeonekana kuwa mlundikanao wa watu wengi hadi kusababisha baadhi ya abiria kuzirai kwa kukosa hewa ya kutosha huku wengine wakigombania kwa kupita dirishani mara yanapotokea.


1 COMMENTS:

  1. Sasa jamani huu si uzembe kwa wahusika wanaoiendesha hii kampuni? Yaani ujinga kabisa labda mpaka rais Magufuli aende kuwaelekeza jinsi ya kutatua tatizo hilo la upungufu wa mabasi? Mambo mengine yanakera hata kuyasikia seuze kuyaona kwa macho yako binafsi. Kwa mwendo huo wa kusuasua wa jongoo kutoka watendaji wa umma mfano hawa viongozi wanaosimamaia mabasi ya mwendo kasi ni dhahiri kuwa watanzania bado tuna safari ndefu. Sifikirii kama hayo mabasi yanatoa huduma bure. Na kama ni mabasi ya kulipia yanayotoza nauli maana yake ni biashara na ni biashara kwa kawaida ndio inayotafuta wateja sio wateja kutafuta biashara ukiona kitu hicho kinatokea wanaofanya biashara katika eneo hilo ni wa wazembe. Transportation industry au huduma ya usafiri ni moja kati ya huduma ambayo wanaohudumiwa huwa ndio kama wamiliki wa huduma na kitendo chochote kitakachosababisha usumbufu kutoka kwa mamlaka husika inayosimamia vyombo vya usafiri husika basi wanatakiwa kutoa suluhusho mbadala la haraka kwa wateja kuhakikisha wanapata huduma yao kama wanavyotarajia. Kwa mfano kama mabasi ya mwendo kasi ni machache kwanini wahusika wasitafute mabasi mengine ya katoa huduma wakati wakiwa na mipango ya kuongeza mabasi zaidi au mpaka yatokee kama yale ya Mv Nyerere? Nina uhakika kama mradi huo wa mabasi ya mwendo kasi ungekuwa ni mradi unaomilikiwa na kuendeshwa na Baharesa na kampuni yao ya Azam basi kusengekuwa na uzembe na adha hii inayoionekana. Labda Serikali ifikirie kuajiri wataalam wa nje kusimamia baadhi ya miradi kwani sio kusimamia tu hutakikana uwepo wa viongozi wenye vichwa venye uwezo wa kubuni makubwa zaidi ila kama kiongozi pesa zinamgombania kuingia kwenye mfuko wake na yeye bado amelala usingizi ujue hapo bado kazi ipo na usifikirie kiongozi au taasisi ya aina hiyo kufanya maajabu yeyote kwani kinachofutaia zaidi ni kufeli na kufa kwa taasisi wanatpiongoza badala ya kupiga hatua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic