October 11, 2018


Kufuatia habari za kutekwa  kwa mfanyabishara maarufu nchini ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji) alfajiri ya leo, Oktoba 12, 2018,  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa,  ametoa taarifa za awali kuwa wahusika wanodaiwa kumteka Mo ni watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

Mambosasa amesema kwamba wakati Dewji anafika kwenye gym ya Colosseum eneo la Oyster Bay jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi, kulikuwa na gari moja lililokuwa limefika kabla na kuegesha mbele yake na jingine lilikuwa nje. 

 Aliendelea kueleza kwamba gari lililokuwa ndani liliashiria kwa kuwasha taa, na lililokuwa nje likaingia ndani na kuegesha mbele ya gari la Dewji ambapo walitoka Wazungu wawili wakambana Dewji na kumuingiza kwenye gari lao aina ya Surf na kuondoka naye kuelekea kusikojulikana.


1 COMMENTS:

  1. Yule mchezaji wa Lyon alietangaza kurudi kwao ulaya yupo vizuri lakini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic