October 11, 2018


Uongozi wa klabu ya Azam FC umewapeleka Afrika Kusini wachezaji wake wawili, Frank Domayo na Paul Peter kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffer Idd Maganga, ameeleza kuwa wameamua kuwapeleka wachezaji hao wakapimwe ili kujua wanasumbuliwa na nini.

Maganga amesema baada ya ripoti za Daktari kutoka, endapo watahitajika kutibiwa klabu itagharamika ili kuwawezesha kupata matibabu ili warudi katika hali zao za kawaida.

Maganga amesema licha ya Domayo kuumia akiwa na timu ya taifa, ameeleza hakua haja ya kuanza kutupia lawama kwa mabosi wa Taifa Stars kuwa wamemtelekeza mchezaji wao na badala yake wao watahusika.

Kauli hiyo imekuja ikiwa na baada ya baadhi ya wadau kulalamika kuwa wachezaji wanapoumia wakiwa Stars wamekuwa wakiachwa ili wasaidiwe na vilabu vyao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic