October 11, 2018


Kikosi cha timu ya Yanga kinatarajia kusafiri kuelekea Zanzibar kesho Ijumaa kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Malindi FC.

Yanga itaenda kucheza na timu hiyo kwa ajili ya kumuaga tena aliyekuwa Nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Yanga imeamua kutoa heshima nyingine tena kwa Cannavaro ambaye hivi sasa ni Meneja wa kikosi cha Yanga baada ya kustaafu soka.

Timu hiyo itaondoka na wachezaji wake wote muhimu ili kutoa burudani ya kutosha visiwani humo kwa ajili ya kumuaga mchezaji huyo.

Cannavaro alipewa heshima ya kuagwa mara ya kwanza wakati Yanga ikiwa imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mechi za ligi kwa kucheza na Mawenzi Market ya Morogoro kabla ya msimu huu kuanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic