October 19, 2018



Mtangazaji maarufu nchini, Isaac Gamba ambaye amefariki dunia mjini Bonn nchini Ujerumani, alifariki takribani siku tatu bila ya watu kujua.

Gamba ambaye alikuwa akifanya kazi katika Kampuni ya Utangazaji ya Ujerumani, Dutche Welle, alifariki dunia siku tatu nyumbani kwake lakini hakuna aliyejua.

“Unajua mimi si msemaji wa familia, lakini Gamba alifariki takribani siku tatu na hakuna aliyekuwa amejua.

“Siku ya kwanza ofisini kwake walimpigia simu ikaita tu, siku ya pili haikuwa imepatikana. Asubuhi siku ya tatu ukafanyika mpango wakaenda na Polisi.

“Walipogonga bila ya mafanikio basi ndiyo wakafikia uamuzi wa kuvunja na kumkuta maskini,” alisema mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani, akiomba asitajwe.

Gamba amewahi kufanya kazi Radio One na ITV na ni mmoja wa watangazaji maarufu wa michezo nchini.

2 COMMENTS:

  1. RIP Isaack Muyenjwa Gamba (Mwanangu) Tutakukumbuka sana. Mbele yetu nyuma yako. Pumzika kwa Amani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic