October 16, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga, umepanga kufanya mchujo wake kwa umakini mkubwa mara tu baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza, uongozi wa Yanga umekuwa ukitaka kupunguza gharama na kuimarisha kikosi chake.

"Gharama ni jambo gumu sana kwa Yanga, lakini viongozi wanajitahidi sana. Hivyo wameanza na suala la gharama halafu wataangalia wale wanaofanya vizuri na vibaya.


"Kama mchezaji hana mchango basi ajue safari itamkuta bila ya kuangalia jina lake. Mchujo utakuwa wa umakini mkubwa," kilieleza chanzo.

Kuhusiana na wachezaji wa kusajili au kuongeza, hilo suala ameachiwa mwalimu kwa kuwa uongozi umeonekana kumuamini.

3 COMMENTS:

  1. Msiwe nyambafu, kumwamini kocha kila anachosema, mlimwamini Lwandamina akawaletea mkata umeme bomu kocha hakuibgia gharama ila nyinyi mliingia fharama, na huyu kamleta kindoki ambae hana huwezo kuzidi baadhi ya makipa wa bongo, nawasihi muwe kuweni makini ila Tambwe na Kamusoko wabaki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Brother naona unakurupuka.....kwanza kocha ndiye mtu sahihi wa kusajili wachezaji anaoona wanafaa kufanyanae kazi.....mnataka mumsajilie mnajua anahitaji wachezaji anaotaka kuwatumia ktk mfumo gani?.Mumsajilie halafu timu ikifanya vibaya mtamlaumu?.Kuhusu issue ya kindoki,huwezi kumpima mchezaji kwa mechi mbili.......alikuja chirwa akaboronga karibia nusu msimu,mbona baadae alikuja kuonyesha uwezo wake?.....Isitoshe unamdharau kindoki nadhani kwakuwa hukumuona kwenye mechi za pre sesson....kwa waliomuona hawawezi kuthubutu kutoa kauli kama hiyo.

      Delete
  2. Huna taaluma ya ukocha unajuaje kama Kindoki hana uwezo?
    Umempima kwa mechi ngapi?
    Acha kuongea usiyoyajua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic