October 16, 2018




Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema mashabiki wa Simba wana nafasi nzuri ya kuishangilia timu yao ya taifa.

Aussems raia wa Ubelgiji amesema kwa Watanzania ni nafasi nzuri kuiunga mkono timu yao wakati ikiivaa Cape Verde kuwania kufuzu Afcon.

"Ni nafasi yao nzuri, ni mashabiki wa Simba lakini Watanzania. Najua watakuwa na jukumu hilo," alisema.

Taifa Stars inashuka dimbani kuivaa Cape Verde ambayo katika mechi iliyopita dhidi ya Stars ilishinda kwa mabao 3-0.

Kiingilio cha chini ni Sh 2,000 ili kuwapa nafasi mashabiki wengi zaidi kuingia Uwanja wa Taifa, leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic