Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ameelekeza nguvu dhidi ya Zimbabwe keshokutwa.
DRC Congo itaivaa Zimbabwe kwao Harare kuwania kucheza Afcon na Zahera ni kocha msaidizi wa Congo.
Zahera ameiambia SALEHJEMBE atarejea na kujiunga na Yanga siku moja baada ya mechi hiyo tayari kuendelea na maandalizi ya ligi.
"Kwa sasa tuko Harare, tunasubiri mechi baada ya maandalizi. Nguvu yote hapa lakini baada ya hapo narudi kuendelea kupambana," alisema.
Kocha huyo Mkongo ameifanya Yanga kuwa imara tofauti na ilivyokuwa ikionekana hapo awali hasa hofu kwa mashabiki kwamba kikosi chao kiko katika hali mbaya sana.
Mbona hutupi matokeo ya mechi ya kwanza huko Kinshasa baina ya CR Congo na Zimbabwe?Au kwa sababu Congo katundikwa 2-1 nyumbani?
ReplyDeleteUsiendeleze tamaa chagua moja Congo National team au Young Africans usilete zako umezaliwa Congo unaishi Ufaransa assistant coac wa Congo at the same time Head coach wa Young Africans ya Tanzania how comes?
ReplyDeleteMambo ya kawaida hata ulaya yapo... mbona hata morocco asistant wa taifa stars n head coach wa singinda... asistant wa italy jee.....? Na wa uruguay jee..... wapo weng
Delete