October 14, 2018





Kocha Patrick Aussems atarejea kazini kesho kuendelea kukinoa kikosi chake.


Aussems raia wa Ubelgiji alitoa mapumziko ya siku moja kwa kikosi chake kabla ya kuendelea kesho na mazoezi.


Bado Simba haijaonyesha cheche kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi lakini Aussems amesisitiza, kikosi chake kitabadili mwelekeo.


Hadi sasa, Simba imecheza mechi saba na iko katika nafasi ya tano ikiwa katika pointi 14.

Kocha huyo Mbelgiji amesisitiza, ligi ni ndefu na wanachotaka ni kuendelea kufanya vizuri mfululizo ili kuhakikisha wanamaliza mzunguko wa kwanza mapema.

1 COMMENTS:

  1. Nasi tunakiamini ndiyo maana tuko na subira ya ubingwa tena viva Simba sc nguvu moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic