October 6, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amelishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia kumpatia tuzo ya kocha bora wa mwezi na kuahidi kupambana zaidi.

Zahera amepatiwa tuzo ya kocha bora wa mwezi Septemba baada ya kufanikiwa kuingoza timu yake ya Yanga kushinda michezo mi­wili na sare mmoja.

Kocha huyo mzaliwa wa DR Congo mwenye uraia pia wa Ufaransa makocha Zubery Katwila wa Mtibwa Sugar na Bakari Shime wa JKT Tanzania

Zahera amezungumza na Championi Jumamosi na kusema: “Ni vizuri kupata tuzo hii, nitawapi­gia simu wakubwa wa TFF kuwaambia asante kwa jinsi walivyonichagua ko­cha bora mwezi huu.

“Waen­delee ku­fanya kazi nzuri kwa roho safi kwa nguvu zote kwa kuwa kitu wa­nachokifanya ni kikubwa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic