November 4, 2018


Leo saa 1 Usiku Yanga itakuwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kukipiga na Ndanda FC katika mchezo wa ligi kuu, habari njema kwa Wanajangwani hao ni kwamba mkali wao wa asisti, Ibrahim Ajibu atakuwa ndani ya dimba.

Ajibu ambaye ana asisti nane na ndiye kinara kwenye ligi kwa asisti, alikosa mechi mbili dhidi ya KMC na Lipuli FC kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Alliance, sasa amepona na alianza mazoezi na wenzake juzi Alhamisi asubuhi.

Ajibu ameeleza kuwa, anashukuru amepona na kuanza mazoezi kwa ajili ya kuipambania namba yake huku akiahidi kuendelea kutengeneza asisti na kufunga mabao katika michezo ijayo ya ligi.

Ajibu alisema, anawashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti kubwa aliyokuwa anaipata kipindi ambacho akiwa anauguza maumivu hayo ya mgongo na sasa yupo fiti baada ya afya yake kurejea kama kawaida.

“Niwashukuru mashabiki kwa sapoti yao waliyokuwa wakinipa wakati nikiwa nje ya uwanja, nilikuwa napokea simu na meseji nyingi za pole na kuniombea nipone haraka ili nirejee kuipambania timu yangu ya Yanga.

“Hivyo, afya yangu hivi sasa imerejea kama zamani na nimeanza mazoezi kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi kwa kuanzia na Ndanda, labda niwaambie Wanayanga kuwa furaha yangu ni kuiona Yanga ikifanya vizuri katika ligi.

“Maneno mengi sana yanasemwa lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. Kwa sasa tunaendelea na maandalizi ya michezo inayofuata na najua changamoto ni kubwa na ligi ni ndefu sana lakini mapambano yanaendelea.

“Achaneni na wanaosambaza taarifa za uzushi na uongo wenye lengo la kutuvuruga wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya kutupunguza morali,” alisema Ajibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic