November 4, 2018


Uongozi wa Yanga umesema kuwa unatambua Yusuf Manji bado mwenyekiti wao hadi pale watakapopokea barua kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya maagizo ya kuitisha uchaguzi mkuu.

BMT, juzi iliitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojizulu huku ikiwemo ya mwenyekiti wao, Manji aliyeiandika barua ya kujiuzulu hivi karibuni.

Taarifa ya BMT kwa vyombo vya habari ilisema kwamba, Yanga imebaki na wajumbe sita kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016, Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten alisema wao suala la kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi mbalimbali ikiwemo ya Manji hawawezi kulizungumzia hilo hadi watakapopata barua kutoka BMT na TFF.

Ten alisema hawana taarifa ya kiofisi waliyoipata kutoka BMT na TFF juu ya agizo hilo huku ukiahidi kulifanyia kazi hilo baada ya kupokea barua kutoka kwenye baraza na shirikisho hilo la soka.

“Nisingependa kulizungumzia hilo la uchaguzi hivi sasa, niwe mkweli kama Yanga hatukupata barua ya kiofisi kutoka BMT na TFF ya kutuagiza kufanya uchaguzi wa baadhi ya wajumbe wa timu na mwenyekiti wetu.

“Nitalizungumza hilo baada ya kupokea barua kutoka BMT na TFF, hivyo nitakavyoweza kusema kwa hivi sasa,” alisema Ten.

1 COMMENTS:

  1. Dah kweli yanga kinganganizi mtu kisha sema hataki nyie kila kukicha mnampigia magoti nyie vipi mbona wagumu wakuelewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic