November 21, 2018

Mchezaji aliyetemwa na timu ya KMC, Humud Abdulhaman amesema kuwa kwa sasa amehamishia makazi yake Tanga kwa muda ili kutuliza akili kutokana na mikasa ambayo amekumbana nayo.

Humud alipigwa chini na KMC kwa kile walichoeleza ni utovu wa nidhamu kwa kuhusika kuwashawishi wake za wachezaji ili aweze kuwa nao kwenye mahusiano pamoja na kuacha vifaa Dar es Salaam wakati timu yao ilipokuwa Tanga.


"Nimeamua kutoka Dar na kuja kukaa Tanga kwa kuwa ni sehemu ambayo imetulia na nitakuwa na amani nikiwa huku tofauti na Dar.


"Siwezi kuacha mpira kwa kuwa najua nina uwezo hivyo najifua mara mbili zaidi kwa siku ili nibaki katika ubora wangu," alisema Humud.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic