November 6, 2018


Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Wizkid, ameripotiwa kununua gari mpya aina ya Lamborghini Urus kwa Naira milioni 101 ambazo ni sawa na Sh. milioni 633.  Habari hizo zinakwenda sambamba na video inayotesa hivi sasa ikimwonyesha katika gereji moja akilikagua gari hilo.

Wizkid hivi karibuni ametoa video yake iitwayo `Fever’,  ambayo ilitusua vilivyo kwenye mtandao wa Intaneti na kutazamwa na watu zaidi ya milioni mbili katika saa zisizozidi 48.



Katika mazingira hayo, amejiunga na orodha ya wasanii wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi duniani hususan pale alipotoa shoo katika moja ya makazi maarufu zaidi duniani —  Umaid Bhawan Palace nchini India.

Katika shoo hiyo alilipwa Rupee milioni 50 ambazo ni sawa na Naira ilioni 245.9, kiasi ambacho hapa nyumbani ni sawa na  Sh. bilioni 1.5.  Katika shoo hiyo kwenye harusi, aliwafanya Wahindi wacheze midundo ya nyimbo zake maarufu kama vile “Soco’’, “Fake Love’’  na nyingine nyingi.

Wizkid alipata umaarufu duniani baada ya kushirikiana na mwanamuziki  Drake wa Canada katika kibao cha  “One Dance”, kilichotinga katika nchi 15 zikiwemo Marekani,Uingereza Canada na Australia.

Alishikia nafasi ya tano katika jarida la Forbes na Channel O kwa wasanii wenye mkwanja mrefu zaidi Afrika na mwaka 2014 akawa mwanamuziki wa kwanza wa Nigeria kuwa na wafuasi zaidi ya milioni moja katika mtandao wa twitter.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic