November 29, 2018


Na George Mganga

Baada ya kusambaratisha vilivyo Mbabane Swallows ya Swaziland kw amabao 4-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi wa Simba umesema safari ndiyo imeanza.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, ameeleza kuwa wamefurahia matokeo hayo lakini akisema inabidi kwa sasa wajipange kuelekea mechi ya marudiano.

Manara ameeleza kuwa wao kama Simba wamejipanga kuwania ubingwa wa Afrika hivyo watapambana kwa namna yoyote ile wawezavyo ili kuchukua taji hilo.

"Safari ndiyo imeanza kwa sasa, tumefurahia matokeo na tujapanga kwa mchezo ujao ili tuweze kusonga mbele na ikumbukwe malengo yetu ni kuchukua kikombe cha Afrika" alisema.

Kauli ya Manara imekuja kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kuwataka Simba wapigane kwa nguvu zote ili walilete taji hilo nchini.

Simba itakutana tena na Mbabane wiki ijayo Disemba 12 2018 huko Swaziland kwa ajili ya mchezo wa marudiano.


1 COMMENTS:

  1. Penye nia hakika pana njia.Na nichukue nafasi hii kuipongeza Simba kwa nia yao Jasiri ya kusema bila ya uoga yakwamba wanataka kuchukua ubingwa wa club bingwa Africa. Na mimi niongezee tu kwa kusema yakwamba Simba nguvu wanayo, uwezo wanao,sababu wanazo na silaha za mapambano wanazo labda washindwe wenyewe ila hata kama wataongezea kidogo silaha za maana za mapambano basi sio mbaya. Nadhani wakati wa wachezaji wa kwenda jaribu bahati zao pale Simba umekwisha kwani simba ni Quality team ni wakati sasa wa Simba kuchukua wachezaji wenye uhakika wakwenda kufanya kazi kama ilivyo kwa mwamba wa Lusaka Cletus Chama.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic