November 29, 2018


Kueleka mechi ya leo ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania, uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwakosa wachezaji wake watano ikieleza bado ni majeruhi.

Kupitia kurasa za timu hiyo katika mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram) Yanga wamewataja wachezaji Juma Mahadhi, Gadiel Michael, Baruan Akilimali, Beno Kakolanya na Kelvin Yondani kutokuwa fiti kiafya.

Uongozi umesema wachezaji hao bado hawajawa fiti kwa kusema kuwa wanasumbuliwa na majeraha, jambo ambalo litawapelekea kutokuwepo kwenye mchezo huo.

Licha ya kutokuwepo, uongozi umewaondolea hofu mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa kueleza mbadala wao utakuwepo.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili na utakuwa mbashara kupitia Azam TV.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic