November 15, 2018




Na Mwandishi wetu
Benki ya TPB imeendelea kuisadia  klabu ya  Waandishi wa habari za michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo ambavyo vitatumiwa na timu hiyo katika michezo yake mbalimbali.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja  Mawasiliano wa  Benki ya TPB Chichi Banda alisema kuwa wamesaidia msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini na muendelezo wao katika shughuli za kijamii ambapo mbali ya michezo, pia usaidia afya na elimu.

Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo mara kadhaa imekuwa ikitwaa ubingwa katika mashindano maalum ya vyombo vya habari yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha.

Alisema kuwa benki ya TPB ni wadau wakubwa wa michezo na mbali ya Taswa SC, pia usaidia timu nyingine.

“Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ” alisema Chichi.

Mwenyekiti waTaswa SC, Majuto Omary aliishukuru benki ya TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwa umakini mkubwa na kushinda katika mechi zao mbalimbali.

“Tunajivunia uwepo wa Benki ya  TPB kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata  mfano  kwa kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha shughuli zake,” alisema Majuto.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic