November 15, 2018


Kocha wa Monaco, Thierry Henry anakabiliwa na presha kubwa kutokana na timu yake kuboronga kwenye Ligue 1. Monaco ilicharazwa mabao 4-0 na Paris Saint- Germain, wikiendi iliyopita kwenye mechi ya Ligue 1.

Henry anakabiliwa na wakati mgumu kutokana na timu hiyo kuboronga kwenye Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Straika huyo, ambaye alianzia soka yake katika timu ya watoto ya Monaco, amekuwa na bahati mbaya ya timu yake kuwa na majeruhi wengi. Monaco ilijikuta ikipokea kipigo cha pili mfululuzo baada ya kufungwa na Club Brugge ya Ubelgiji kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mechi dhidi ya PSG, mabao matatu yalipachikwa na Edinson Cavani wakati Neymar alifunga kwa penalti. PSG Inaongoza kwa pointi 13 kwenye Ligue 1, wakati Monaco ipo kwenye nafasi za mkiani kwenye ligi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic