November 1, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepewa majukumu ya kuhakikisha linasimamia uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga ambao limeagiza ufanyike.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Alex Kenyenge wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

Kenyenge ameeleza hayo huku akiitaka klabu hiyo kuhakikisha inajaza nafasi ya Yusuf Manji ambaye alipitishwa na wanachama wake kuendelea na wadhifa huo licha ya kuandika barua ya kujiuzulu.

Manji ambaye kwa muda mrefu amekuwa kiongozi ndani ya Yanga, alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti, lakini wanachama wa Yanga walikataa uamuzi wake huo.

Wakati mchakato wa uchaguzi huo ukisubiriwa kuanza, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilikuwa halitambui kujiuzulu kwa Manji kitendo ambacho kilitafsiriwa kwamba bado ni mwenyekiti wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic