Kucheza ndio kushinda na ndio maana ukicheza na timu ya ushindi SportPesa una nafasi kubwa ya kuondoka na bajaj mpya kabisa. Huu ni msemo maarufu unaotumiwa na wachezaji wa kampuni ya SportPesa unaomaanisha ni lazima ucheze ndio ujipatie nafasi ya kushinda.
Shija Kado (28) kutoka Kivule jijini Dar es salaam ni mshindi wa droo ya 37 ya Shinda Zaidi na SportPesa amekabidhiwa bajaj baada ya ushindi na kama kawaida simulizi za ushindi zilipata nafasi.
Akielezea furaha yake mara baada ya kukabidhiwa bajaj yake katika eneo la mbagala zakhiem, kado alisema huu ni ushindi mkubwa katika historia ya maisha yake maana hajawahi kufikiria kama siku moja moja anaweza kushinda.
Mshindi huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi anasema kuwa tangu ameanza kucheza ni muda sasa na kushinda bajaj hiyo kwake ni kama hesebu zake zimekaa sawa maana rasmi anaanza mchakato wa kutengeneza njia mbadala itakayomuwezesha kuzitunza fedha zitakazotokana na bajaj hiyo ila kuandaa mradi mkubwa utakaomuinua zaidi kiuchumi.
"Daaah kweli sasa sitategemea mshahara tena maana kupitia bajaj ntaingiza kipato kingine tena kinaweza kuwa kikubwa kuliko hata mshahara na kitanisaidia mimi na familia yangu. Hata mke wangu wakati nacheza hakupenda kabisa ila nilipomwambia nimeshinda yeye ndio wa kwanza kushangilia na sasa ivi ndio ananisisitiza kucheza kila siku maana kaiona bajaji sasa" alisema Kado.
Kwa upande Wake Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Kutoka SportPesa Tarimba Abbas akimkabidhi mshindi huyo bajaj alisema kuwa bado watanzania wana muda wa kutosha kucheza na SportPesa maana ushindi upo njenje huku akiongeza kuwa mbali ya kushinda bajaji unaweza kushinda mamilioni ya Jackpot sambamba na safari ya kwenda Uingereza au Hispania kushuhudia mitanange ya ligi ya nchi hizo.
Piga *150*87 kupitia simu yeyote ya mkononi ambapo hapo utafanikiwa kujisajili na timu ya ushindi na kuanza kucheza lakini pia unaweza kucheza kupitia www.sportpesa.co.tz na kumbuka kuwa kucheza mara nyingi ndio kuongeza nafasi ya kuibuka mshindi.









0 COMMENTS:
Post a Comment