BODI YA LIGI YATOA TAMKO LA KIBABE KUHUSIANA NA DIRISHA DOGO
Na George Mganga
Baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa jana, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi kupitia TFF, Boniface Wambura, amesema hakutakuwa na siku za nyongeza juu ya usajili wa wachezaji.
Wambura ameeleza hayo kutokana na utamaduni wa timu za kitanzania kuchelewa kufanya usajili wa wachezaji wakiamini kutakuwa na siku za nyongeza hapo baadaye.
Mkurugenzi huyo amesema katika mfumo huu mpya unaotumika kwa sasa maarufu kama TFF FIFA CONNECT hauna cha kuongeza muda hivyo kwa timu ambazo zinategemea ofa hiyo zisahau.
Dirisha limefunguliwa jana Novemba 15 ambapo litadumi mpaka Disemba 15 2018 wakati huo mechi za ligi zikiwa zinaendelea kama kawaida.
Tayari klabu kadhaa zimeshaanza kupigania saini za wachezaji wapya ili kujaza mapungufu ambayo yanazikumba timu zao.








TFF na bodi ya ligi mna mapungufu ya wazi ambayo hata mtoto mdogo ukimueleza atashangaa sana,hivi inawezekana vip timu iliyocheza mechi tofauti na nyingine mziweke kwenye kinyang'anyiro au ushindani??kama TFF mmeamua kumtafuta kocha bora ni bora mfanye haki,timu zinatakiwa zicheze idadi sawa ya michezo sio simba kacheza mitatu unamlinganisha na azam aliyecheza mechi nne kweli inaingia akilini hiyo??kwa mtazamo wangu finyu naona wazi kwamba hapo kuna makosa,ni sawa na ligi iishie kwa lipuli kupewa ushindi kisa kucheza mechi kumi nakushinda zote kwa goli moja,wakati azam amecheza mechi Tisa na kashinda zote kwa goli tatu,sasa kwanini usimpe azam acheze mechi yake ya kumi then ndio mtafute mshindi.acheni kufanya mambo kwa upendeleo.mpira hautaki hivyo jamani.
ReplyDeleteEti Hans van pluijim ampiku Patrick ausem.acheni hujuma nyie kwanini msimpunguzie azam mechi mkahesabia mechi tatu ndio mumtafute kocha bora.mmependelea kwasababu ya uzembe wa kanuni zenu hapo aliyestahili ni kocha wa simba na kama siyo basi mngewaruhusu simba wacheze mechi sawa na azam then ndio mumtafute kocha bora,but kiuhalisia hata mfanye nini mbelgij wa simba ni hatari na ndiye aliyestahili tuzo kwa mwezi tajwa.sahihisheni makosa hapa mlichemka.
ReplyDeleteUkizingatia simba wamekua wakiomba sana suala la wao kuruhusiwa kucheza mechi ilimradi kupunguza viporo but TFF hamlioni hilo sijui why then leo mnakuja kutuletea mchakato ambao haueleweki tuwaelewe vp sasa.
ReplyDeleteUkizingatia simba wamekua wakiomba sana suala la wao kuruhusiwa kucheza mechi ilimradi kupunguza viporo but TFF hamlioni hilo sijui why then leo mnakuja kutuletea mchakato ambao haueleweki tuwaelewe vp sasa.
ReplyDelete