November 9, 2018


Baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Azam FC, Mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa, amesema kuwa haoni shida kuvunja mkataba pale stahiki zake zinapokuwa hazilipwi.

Mchezaji huyo ameeleza kuwa kwake jambo hilo ni la kawaida wala huwa hapepesi macho kufanya maamuzi hayo akisema ana familia ambayo inamtegemea.

Chirwa ambaye aliwahi kuichezea Yanga, amesema anawashangaa wachezaji wengi hapa nchini kutokana na kushindwa kuwa na misimamo jambo ambalo linawafanya waendelee kuzipigani timu zao bila kulipwa chochote.

"Unajua wachezaji wengi hapa nchini wamekosa msimamo wa kulinda mikataba yao, niko tayari kuvunja mkataba wangu na kwenda mahala pengine ninapoona stahiki zangu hazilipwi kwasababu nina familia na inanitegemea" alisema.

Mchezaji huyo alirejea nchini hivi karibuni na kuelezwa angesajiliwa na Yanga lakini Azam wakaja na dau nono kisha wakamsajili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic