November 9, 2018


Na George Mganga

Mratibu wa timu ya Yanga, Hafidh Saleh ameibuka na kusema kuwa ni kweli jumla ya wachezaji wanne hawakufika mazoezini juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini.

Saleh ameeleza kuwa wachezaji walishindwa kufika kutokana na matatizo mbalimbali yaliyowakwamisha na kushindwa kufanya mazoezi.

Wachezaji hao ambao ni Andrew Vincent, Ibrahim Ajibu, Matheo Anthony na Mrisho Ngassa, walishindwa kujumuika katika mazoezi ya juzi na kuzua maswali kwa wanayanga baada ya taarifa zao kuenea.

Saleh amesema mchezaji kama Ajibu bado hajapona vizuri akieleza alikuwa kwenye matibabu huku Matheo aliaga kwenda kwenye msiba wa ndugu yake.

Yanga inaendelea kujifua hivi sasa kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara ambapo katika mchezo unaofuata itakuwa inakabiliana na Mwadui FC huko Shinyanga.

1 COMMENTS:

  1. Nampongeza Zahera,Kwa misimamo juu ya nidhamu kwachezaji jambo LA nidhamu asiachiwe cocha pekee iwe na uongozi wrote.msifichefiche udhaifu,maana msiba utakuja kuwaumbua.Kwanza wachezaji waelewe kuwa Moira Kwa sssa ni ajira na sio kudekadeka na uringa.wachezaji lazima waitendee haki klabu yso,wameajiliwa Kwa kufuata vipaji vyao,na basis vionyeshwe wazo ikiwa pamoja na nidhamu.Kwani inakuwaje ikiwa inatokea clabu kuvhelewesha malipo ya mchezaji.bilashaka mchezaji yule ataumia.Basis Sasa kadhalika mchezaji asipotimiza wajibu waka kazini ,club inaumia maana itamlipa MTU ambaye hakutimiza wajibu wake na hasara huingizwa na mchezaji hiyo.Basis viongozi wasiwachie makocha tu kudhibiti nidhamu.wala wasione kuwa watamuuzi mchezaji.wakaze Uzi,na mvhezaji ajielewe.ni mwajitiwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic