November 4, 2018


Msanii wa Hip Hop Bongo, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’, ametinga katika Kituo cha Polisi cha Oyster Bay jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa jeshi hilo ikiwa ni siku chache baada ya kuanika hadharani majina ya watangazaji wa kiume wanaojihusisha na vitendo vya ushoga.

Akizungumza wakati wakielekea Polisi, Dudu Baya amesema: “Naelekea Kituo cha Polisi Oysterbay, kama nikiwekwa ndani kwa ajili ya hawa mashoga.

"Sitaki ndugu yangu yeyote aniletee maji wala chakula, nitashinda na kulala njaa mpaka niimalize hii kazi ya Mungu, AMEN.”

Dudu Baya ambaye anajiita Mamba au Oil Chafu Konki Konki Konki Master amefika Oyster Bay Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni kuhusu orodha ya majina ya watu aliyoitoa mtandaoni akidai wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic