HAJI MANARA AJA NA USHAURI WA BURE KWA YANGA JUU YA UCHAGUZI
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameamua kutoa ushauri wa bure juu ya watani zao wa jadi Yanga kuendelea kumtaka Mfanyabiashara Yusuf Manji awe Mwenyekiti wao.
Manara ameeleza Yanga hawapaswi kumlilia mtu mmoja pekee na badala yake ameshauri waanzishe mfumo wa mabadiliko kama ambao Simba wanaelekea kuukamilisha hivi sasa.
Msemaji huyo mwenye maneno mengi amewaambia Yanga wawaige Simba kwani wao hawamtegemi mtu mmoja bali wanategemea muundo wa mabadiliko.
Hatua hiyo imekuja kufuatia idadi kubwa ya wanachama Yanga wamekuwa wakipinga kufanya uchaguzi wakidai kuwa bado wanamtambua Manji kuwa ni Mwenyekiti wa klabu.
Kutokana na Yanga kuonesha dalili ya kutotaka kujaza nafasi yake ya Uenyekiti, Manara amewashauri ni vema wakaufanya kisha waanze mchakato wa mabadiliko ya klabu kwenda kwenye uwekezaji.
"Hawa wenzetu wamekuwa wanamtegemea mtu mmoja, imekuwa ni tatizo kwao, ni vema wakaanzisha mfumo mpya kama tulionao sisi kwa maana hatutegemei mtu mmoja" alisema.
Kwani Manara kukaa bila kuizungumzia yanga atakufa au? Hebu iache yanga ina msemaji wako duh yaani unakiherehere kweli!
ReplyDeleteHivi huyu jamaa ni msemaji wa Yanga au?
ReplyDeleteWakati mwingine nashawishika na conspiracy kwamba kiasili huyu jamaa ni Yanga ila Simba yuko kikazi
hata mm nahisi hivyo huyu jamaa ni msanii namba moja
Delete