November 15, 2018


Na George Mganga

Wakato dirisha la usajili nchini likiwa limefunguliwa rasmi leo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, tayari ameshawasilisha ripoti ya wachezaji anaowahitaji wasajiliwe.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema kwa sasa yupo mafichoni akiwasaka wachezaji hao kimyakimya ili kukiboresha kikosi cha timu hiyo.

Ripoti ya Zahera imeeleza anahitaji beki mmoja ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi atakayesaidiana na Nahodha Kelvin Yondani sambamba na Andrew Vincent 'Dante'.

Aidha, ripoti imehitaji washambuliaji pamoja na nafasi ya winga wa pembeni ili kuiongezea makali zaidi timu baada ya kuwa na uhaba wa mabao haswa tangu kuanza msimu huu.

Nyika amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kutokuwa na wasiwasi juu ya usajili ambao wanaenda kuufanya hivi sasa kwani anaamini utakuwa wa nguvu na wa uhakika.

6 COMMENTS:

  1. Endeleeni kusajili kwa siri mtuletee akina kindoki

    ReplyDelete
  2. Je waliopo wameshapata haki zao? Naamini Waziri mwenye dhamana na michezo akishirikiana na TFF watafanya usajili wa maana safari hii kuisaidia Yanga iwe timu imara kuliko wanachama wake. Binafsi naona mgogoro mkubwa ukifukuta Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic