November 4, 2018


Timu ya Azam FC iliyo chini ya Hans Pluijm imefanikiwa kujikita kileleni kwenye msimamo baada ya kufanikiwa kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo mpaka sasa wakiwa wamecheza michezo 12.

Ushindi huo unakuwa ni wa tatu mfululizo kwa Azam wakiwa ugenini walianza kushinda mbele ya JKT Tanzania kisha Singida United na leo mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba.


Michezo yote mitatu Azam wameshinda kwa bao 1 pekee  huku mshambuliaji wao Donald Ngoma akihusika kwenye mabao yote akifunga mawili na kutoa pasi moja katika mchezo wa JKT Tanzania na amefikisha mabao 3.


Ngoma ataukosa mchezo ujao wa Azam kwa kuwa ana kadi nyekundu ambayo ameipata leo dakika 90 baada ya mwamuzi Shomari Lawi kutafsiri kuwa amefanya kitendo kisicho cha kinidhamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic