November 15, 2018


Kocha mkuu wa Azam FC, Hans van Pluijm ameibuka na kusema kwamba anachokifanya yeye ni kuzimaliza timu za Simba na Yanga kimyakimya kwa kusajili wachezaji ambao wataiwezesha klabu hiyo kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Kocha huyo amesema hayo zikiwa zimepita siku chache baada ya klabu hiyo kumalizana na mshambuliaji Obrey Chirwa ambaye ametua kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji la klabu hiyo.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Pluijm raia wa Uholanzi amesema ; “Sisi tunachofanya ni kusajili wachezaji wetu kimyakimya ambao watakuwa msaada kwetu kwenye kupambana na kufikia malengo tuliyojiwekea ya kutwaa ubingwa kwa msimu huu.”

“Sisi ni tofauti na Simba na Yanga ambao wao wenyewe wamekuwa wakisikika kila mara kwamba watamsajili huyu na yule, sisi hatutaki kwenda hivyo tunakaa kimya lakini tunachukua nyota ambao watatusaidia,”alisema Mholanzi huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic