November 15, 2018


Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameutaka uongozi wa timu hiyo kutuma watu ambao wataenda kuwasoma wapinzani wao, Mbabane Swallows kwa lengo la kupata urahisi kwenye mechi la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba watacheza na Mbabane Swallows katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wataanzia nyumbani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kati ya Novemba 27 au 28, kabla ya kurudiana Swaziland.

Chanzo kutoka katika klabu hiyo kimeliambia Championi Jumatano, kwamba kocha huyo ametaka uongozi wakaipeleleze Mbabane kwa ajili ya kujua namna gani ambavyo wanacheza na mbinu gani wanatumia.

“Kocha kataka mtu aende kule Swaziland kwa ajili ya kuwaangalia wapinzani wetu kisha kumpa ripoti ya namna ambavyo wanacheza na masuala mengine ya kiufundi.

“Anataka kufanya hivyo kwa sababu ya kupata urahisi kwenye mechi ya hapa nyumbani na kuimaliza kabisa kabla ya kwenda kwenye mechi ya ugenini,” kilisema chanzo hicho.

Championi lilimtafuta kocha huyo ambapo alisema: “Siwajui wapinzani wetu ila ninajua watakuwa wazuri, tunatakiwa kuwaangalia kwa ajili ya kuwatazama kwa namna ambavyo wanacheza ili tumalize kazi tukikutana nao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic