November 5, 2018


Uongozi wa timu ya Alliance umesema kuwa kazi kwao ndo imeanza ligi kuu hivyo wataendeleza moto wa ushindi kwa kila timu itakayoshuka katika uwanja wao wa nyumbani Nyamagana, mkoani Mwanza.

Ofisa habari wa Alliance FC , Juma Mwafulango alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo chanya ili kuonyesha tofauti waliyonayo kwenye ligi.


"Unapozungumzia Alliance FC, tambua kuwa ni timu ambayo inacheza mchezo wa darasani na wachezaji wana uwezo mkubwa na juhudi hasa wakiwa uwanjani kutafuta matokeo, tayari wamekwisha kuanza kuelewa wanachotakiwa kukifanya mambo mazuri yanakuja," alisema.


Mchezo uliopita Alliance walifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Singida United katika Uwanja wa Nyamagana mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar ambao nao watawafuata Nyamagana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic