November 5, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Prisons, Abdallah Mohammed amesema kuwa kinachowafanya washindwe kupata matokeo kwa sasa ni kutokana na kushindwa kuwa na washambuliaji makini.

Msimu uliopita Prisons walifanikiwa kufanya vizuri kwenye ligi baada ya kumaliza wakiwa nafasi ya nne hali iliyofanya akafanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa msimu kwenye ligi kuu.


"Tunashindwa kupata matokeo kutokana na washambuliaji kukosa umakini hasa kwa nafasi ambazo wanazitengeneza kushindwa kuzitumia hali ambayo inafanya tushindwe kushinda, hilo tumeliona na tunalifanyia kazi ili kuweza kurekebisha makosa," alisema.


Prisons alilikubali sare ya kutofungana na timu ya Mwadui jana katika uwanja wa Mwadui na kufanya wagawane pointi moja, Prison wanaendelea kushika nafasi ya 19 wakiwa na pointi 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic