November 5, 2018


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga Ibrahim Ajibu bado amedhihirisha kwamba yeye ni fundi wa kutoa pasi za mwisho za mabao kwenye ligi kuu akiwa amefikisha pasi tisa kwa sasa.

Ajibu amerejea kwenye ubora wake na alikosa michezo miwili ambayo Yanga walicheza dhidi ya KMC na Lipuli kutokana na kuumia mgongo katika mchezo wao dhidi ya Alliance.


Kiungo huyo ambaye ameweza kufunga mabao matatu kwenye timu yake ya Yanga pia aliwahi kuchezea timu ya Simba kabla hajajiunga na timu ya Yanga.


Yanga wamecheza michezo 10 na wamefanikiwa kushinda michezo nane na kutoa sare michezo 2 yote wakiwa wamecheza uwanja wa taifa Dar es Salaam wakiwa na pointi 26 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic