November 16, 2018



Licha ya kutoka sare ya kutofungana, dakika 83 alizotumia uwanjani, kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Niyonzima katika mchezo wa leo dhidi ya Nyasa Big Bullets zinatosha kuonyesha bado ananafasi ya kuisaidia Simba.

Niyonzima ameweza kutengeneza zaidi ya mashambulizi mawili leo katika uwanja wa Taifa ambapo timu yake ilikuwa ikicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Nyassa Big Bullets ya kutoka Malawi.

Amepiga kona mbili na zote zilikuwa zikiwafikia wachezaji tatizo likawa kwa umaliziaji na alifanikiwa kupiga shuti kali nje ya 18 dakika ya 74 likakwama kwenda langoni kutokana na hesabu kukataa.

Alitoka dakika ya 83 nafasi yake ikachukuliwa na Marcel Kaheza, mchezo huu ni wa kwanza wa kimataifa kwa Simba baada ya ratiba ya Ligi ya Mabingwa kupangwa, ambapo Simba watacheza na Mbabane Swallows ya kutoka Swaziland Novemba 28, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic