November 16, 2018


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameambulia sare ya bila mabao dhidi ya wageni wake, Nyassa Bullets kutoka Malawi.


Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba walipoteza nafasi kadhaa za wazi.

Hata hivyo, wakati mwingine kipa, Deogratius Munish ‘Dida’, alilazimika kufanya kazi ya ziada kuzuia michomo ya wachezaji wa Bullets ambao walionyesha ni hatari.




Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems aliamua wachezaji wake wapate mechi za kujipima nguvu hasa kwa wale ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa.

Simba ilionyesha kiwango kizuri katika mechi hiyo lakini tatizo la umaliziaji likaonekana kuiandama.




1 COMMENTS:

  1. Heri ya Simba...kwa ni Yanga waliponea chupuchupu kufungwa na timu ya daraja LA kwanza!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic