Tatizo la umaliziaji kwa nafasi ambazo wanazipata bado limeendelea kuwamaliza Simba kwa kuwa walifanikiwa kuwa na umiliki wa mpira na kufanya mashambulizi ya hapa na pale katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets ya kutoka Malawi.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam leo, umemelizika kwa timu zote kutoona lango la mpinzani na kufanya takwimu ziwe kama ifuatavyo:-
Mashuti yaliyolenga lango:- Simba 3- 1 Nyasa Big Bullets.
Mashuti yasiyolenga lango:- Simba 7-6 Nyasa Big Bullets.
Kona :- Simba 3-1 Nyasa Big Bullets
Faulo :- Simba 13- 18 Nyasa Big Bullets.
Kuotea: Simba 2-3 Nyasa Big Bullets.
Kadi za njano:- Simba 1- 2 Nyasa Big Bullets.
Umiliki wa Mpira :- Simba 56- 44 Nyasa Big Bullets.








0 COMMENTS:
Post a Comment