November 9, 2018


Kocha  Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuwa  atajitahidi kuhakikisha wachezaji wake wote wanacheza, hivyo yule atakayeonyesha juhudi atapata nafasi ya kuanza.

Mchezo uliopita dhidi ya JKT ambao ulichezwa uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, Adam Salamba na Claytous Chama hawakucheza licha ya mashabiki kuwa na shauku ya kuwaona ndani wakionyesha ujuzi wao.

"Kikosi cha Simba kina wachezaji wengi wazuri na wana uwezo mkubwa, ili kuweza kucheza ni lazima kila mmoja aonyeshe juhudi na nitahakikisha wote wanaweza kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wao.

"Wachezaji wanajua, pia kanuni zipo wazi ni lazima nianze kuwatumia wachezaji 11 tu, hivyo kila mmoja kwangu ni bora, sioni taabu kumuweka benchi mchezaji yoyote iwe ni Kagere, Bocco hata Okwi wote ni wachezaji wa Simba," alisema.

Ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba umekuwa mkubwa hali ambayo inafanya wachezaji wengi kuishia benchi, pia wapo wengine ambao hata nafasi ya kukaa benchi hawana.

2 COMMENTS:

  1. Ligi Kuu ina timu 20, hivi habari ni za makocha wa Simba na Yanga tu. Tupeni habari za timu nyingine tujue radha yake.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakisema waandike habari za timu nyngn zinasikitisha utaskia hawana posho mara nauli huku kelele wachezaji wanakosa mishahara yani ghasia tupu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic