November 24, 2018


Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara watacheza na timu ya Mbabane Swallow FC katika mchezo wa fainali za Ligi ya Mabingwa Novemba 28 katika uwanja wa Taifa wamepewa tahadhari mapema na kocha aliyewafunga Mbabane.


Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche amesema kuwa walifanikiwa kucheza nao katika ligi ya Mabingwa mwaka 2007 katika uwanja wa Chamazi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 hivyo Simba wanapaswa kuwa makini.


 Cheche amesema kuwa kikosi cha Simba kipo imara ila bado hakipaswi kuamini kinaweza kupata matokeo mbele ya Mbabane ambao wana mbinu wakiwa nje ya uwanja na ndani ya uwanja.

"Kikubwa ambacho Simba wanatakiwa kufanya ni kudhibiti mashambulizi yao hasa wakiwa ugenini huwa wanashtukiza ili kupata matokeo kwa kuwa hesabu zao ni kupata sare ugenini ila ukienda nyumbani kwao hawawezi kukuacha salama.


"Ili wafanikiwe kupata matokeo wahakikishe wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kuwafunga kadri wanavyoweza kifupi kazi yao kubwa inabidi wamalizie kwenye mchezo wao wa nyumbani, watakapowafuata wajiandae kisaikolojia hasa kwa fitina zao ili waweze kupata matokeo chanya," alisema Cheche.


Azam FC walishinda mchezo wa nyumbani ila walipowafuata Mbabane, Swaziland walifungwa mabao 3-0 hali iliyowafanya watolewe mwanzo kabisa wa mashindano hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic