November 3, 2018


Na George Mganga

Mambo mawili yaliyofungwa na Meddie Kagere katika dakika za 11 na 38 kipindi cha kwanza yameiwezesha Simba kung'ara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Simba ilimuazisha kiungo wake Mghana, James Kotei ambaye alikuwa anatumikia adhabu kufuatia kumpiga Gadiel Michael katika mechi ya mwisho iliyowakutanisha watani wa jadi.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuikimbiza Azam FC iliyo na pointi 27 kileleni kwa kufikisha alama 26.

Licha ya ushindi huo, Kocha Patrick Aussems ameulalamikia Uwanja wa Mkwakwani kuwa si rafiki kwa kuchezea na akiomba kama kuna uwezekano uweze kufanyiwa ukarabati.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic