Langalanga ameamua kujivua kutokana na kurejea kwa Yusuf Manji ambaye alitangaza kujizulu takaribani mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa imepita.
Kujivua kwa Langalanga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kumemfanya afunguke kuwa yeye anamkubali Manji hivyo hana haja ya kuendelea kushikilia nafasi hiyo.
Kupitia Baraza la Wadhamini Yanga, Mwenyekiti wake, George Mkuchika, alisema Manji ameandika barua ya kuomba kurejea kwenye nafasi yake hivyo hakuna tena haja ya kujaza nafasi ya Uenyekiti.
Kuelekea uchaguzi wa Yanga utakaofanyika January 13 2019, Yanga itafanya uchaguzi wa kujaza nafasi zingine zilizo wazi ikiwemo baadhi ya nafasi za Kamati ya Utendaji, Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti.








0 COMMENTS:
Post a Comment