November 15, 2018


 

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera anahitaji kuongeza wachezaji wake kwenye kikosi cha Yanga hasa kwa nafasi ya ushambuliaji ili kuwa na makali kwa kushirikiana na Herieter Makambo, mpachika nyavu namba moja Ligi Kuu Tanzania Bara, Eliud Ambokile amewapa masharti mazito.

Ambokile ambaye anaitumikia Mbeya City, amekuwa akihusishwa kutua Yanga dirisha dogo ambalo limefunguliwa leo, amempiga bao mshambuliaji wa kimataifa Meddie Kagere kwenye ufungaji wa mabao akiwa na mabao 8 huku Kagere ambaye akiwa na mabao 7.


"Kama Yanga wanahitaji saini yangu ni lazima wahakikishe nina weza kupata namba katika kikosi cha kwanza kama ilivyo hapa Mbeya City ili nizidi kuisaidia timu na kukuza kiwango changu, nina malengo ya kuweza kucheza soka ligi ya Ulaya iliyo bora.


"Wanapaswa  kuongea na uongozi ili waweze kukubaliana kwanza maana mimi nimesajiliwa kutoka Wenda FC kwa utaratibu na bado nina mkataba hapa hivyo kama wanahitaji huduma yangu wafuate masharti, kisha mimi nitacheza sina tatizo na uwezo wangu.


Uongozi wa Mbeya City ulisema kuwa kama Yanga wanahitaji saini ya Ambokile basi wakunjue pochi kwa kupeleka mkwanja usiopungua milioni 50 ili kupata saini ya nyota huyo mwenye kiduku kichwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic